UTARATIBU WA KUOMBA KIBALI CHA KUTUMIA MAJI JUU NA CHINI YA ARDHI
- Barua ya maombi
- Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha katika ofisi ya Bonde (Iringa, Rujewa-Mbeya, Ifakara-Morogoro, au Utete-Rufiji) ikiambatana na ada ya maombi. Ombi husika, ada hizi hutofautiana kutokana na aina ya matumizi ya maji.
- Ombi hutangazwa kwenye gazeti la serikali na tangazo hilo huwekwa kwenye mbao za matangazo kwa wakuu wa wilaya husika. Bodi itaomba maoni kutoka kwa watumiaji wa chanzo hicho ambapo wanaweza kuathirika kama ombi litakubaliwa. Pia itaomba maoni kutoka Halmashauri husika. Kwa miradi mikubwa hadi uthibitisho wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) huitajika kwa ajili ya athari za kimazingira na kijamii.
- Ofisi kukagua eneo la chanzo cha kuchukulia maji na kuchukua sampuli ili kujua ubora wa maji hayo.
- Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009, baada ya siku arobaini kupita tangu kuombwa kwa maoni na kutangazwa kwenye gazeti la serikali, ombi linaweza kufikishwa katika kikao cha Bodi ya Maji ya Bonde.
- Kibali hutolewa kwa maombi yaliyoidhinishwa na kikao cha Bodi. Mkurenzi wa Bonde ambaye pia ni katibu wa Bodi ya Maji ya Bonde anaweza kutoa au kutotoa kibali kufuatana na maelekezo ya Bodi.
- Kwa maombi yaliyokataliwa, waombaji wana haki ya kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana na maji.
VIAMBATANISHI
Fika ofisi zozote za Bodi ya Maji Bonde la Rufiji na utajaza form kulingana na ombi unalohitaji, aina ya “form” za maombi ya vibali ikiambatanishwa na taarifa zifuatazo: -
A. MAOMBI YA KIBALI CHA MATUMIZI YA MAJI.
- Barua ya maombi
- Ripoti ya uchimbaji kisima, ikionyesha kina (urefu wa kisima) na uwezo wa kisima.
- Ripoti ya uchuguzi wa maji juu ya ardhi (Hydrological Survey Report)
- Ripoti ya maabara, ikionyesha “ubora wa maji”
B. MAOMBI YA KUTIRIRISHA MAJITAKA
- Barua ya Maombi
- Ripoti ya maabara, ikionyesha kiwango cha maji yanayotupwa
- Leseni ya biashara
- Leseni ya makazi
- Kibali cha ujenzi
- Kibali cha uzalishaji
- Kiwango cha uzalishaji
- Cheti cha Uthibitisho wa Mazingira
- Cheti cha Ukaguzi wa Mazingira
- Ripoti ya Mwisho ya Ukaguzi wa Mazingira
C. MAOMBI YA KUCHIMBA KISIMA
- Ripoti ya Survey