
Katika kuimarisha shughuli za ufuatiliaji wa Rasilimali za maji kidigitali ndani ya Bonde la Rufiji Wizara ya Maji imekuja na mfumo wa kisasa zaidi utakaotumia Satelaite katika ukusanyaji wa taarifa za Hali ya hewa na hali ya maji katika mito ili kuendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya rasimali hiyo kisasa zaidi.
Ujenzi wa mfumo huo unaojengwa na kampuni ya SEBA and TDS JV ya Ujerumani unatarajia kuwa mwarobaini katika utunzaji wa takwimu za maji kutokana na ubora wa vifaa vinavyosimikwa katika eneo la bonde
Kwa mujibu wa Mtaalamu wa Haidrolojia kutoka Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Ally Diwani ambaye pia ndiyo mtaalamu na msimamizi wa mradi huo amesema bonde la rufiji limepata vitua 46 vitakavyojengwa ili kusaidia kupima hali ya maji yaliyo juu na chini ya ardhi.
“Kwasasa kazi inayoendelea hapa ni ufungaji wa antena(dishi) kwaajili ya ukusaji wa taarifa zinazotoka kwenye vituo,hili ni dishi la Satelaite ni mfumo wa kisasa na ni bora kwa ukusaji wa takwimu za maji”alisema