Karibu

Karibu kwenye tovuti ya Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji.Katika Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji, tumejikita kuhakikisha usimamizi endelevu, uhifadhi, na ugawaji wa rasilimali za maji kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kupitia ushirikiano na jamii, taasisi  za Serikali na wadau mbalimbali, tunatengeneza mizania ya usimamizi wa rasilimali za maji ambayo inanufaisha watu, mazingira, na shughuli za kiuchumi. Dhamira yetu ya utunzaji inachochea juhudi zetu za kukuza, kuratibu na kutekeleza usimamizi jumuishi wa rasilimali za maji katika Bonde hili. Asante kwa kutembelea tovuti ya Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji, kwa pamoja tunaweza kuhakikisha "kila tone lina thamani"